Thursday, October 27, 2011

Nawakumbuka marafiki zangu.

Kutoka  kushoto, Mimi,  Michael,  Said  na Emmanuel katika moja ya hafla tulipokuwa chuoni (May 2011)






Ni   wakati   mwingi   sana  tulikuwa  pamoja katika kufanikisha lengo letu la kisomo cha elimu ya juu pale chuoni. Hakika ni suala jema hasa pale tulipomaliza  salama  ila  ilikuwa  ni  sala  zaidi  kwa   kuwa  Mungu alikuwa  pamoja  nasi  katika  kipindi  kile  chote  na  hata  ushirikiano  tulioonyesha  baina  yetu  kama ndugu na naamini  tumejenga  undugu mzuri  tu ambao  utadumu daima na Mungu atutangulie katika lyote  hasa katika ngwe  hii mpya  ya maisha.
Kaka  Michael  Filbert,  Emmanuel  Kasenga ,  Said  Bakema,  Fidelis  Choga  kiukweli mmekuwa chachu kubwa na nimejifunza mengi  kupitia  kwenu na  hayo naamini nitayafanyia kazi na kuyaendeleza   popote pale  nitakapokuwa. Pia nawashukuru hata marafiki zangu wapendwa wengi tu japo siwezi kuwataja wote ila  ni pamoja na France, Maiko, Said Kingu, Abraham, Willy, Pius, Stanley, Samwel, Gidion, Janeth, Leticia, Ramla, Rachel, Teddy, Debora, Emmy, Naumi, Noela, Tunsume, Julie, na  wengineo wengi sana  na bila kusahau makundi mbalimbali niliyofanikisha  kufanya nayo  mijadala mbalimbali  juu  ya  masomo.  I  do  remember you and  i  love u so so much and keep intouch . Much   blessings  and  all the  best.

Sunday, October 23, 2011

MICHEZO WIKIENDI.


 HAPA NYUMBANI.

Hapa nyumbani tambo za kuutafuta ubingwa wa ligi kuu bado zinaendelea kwa timu kadhaa kuzidi kutafuta nafasi ya kuwa mabingwa japo bado imeonekana dhahili kuwa ni timu ya Simba na Yanga ndizo zinazidi kujikita kileleni baada ya zote kupata ushindi wikiendi hii na kuzifanya kuwa katika hali nzuri zaidi hasa katika kipindi hiki zinapotegemewa kukutana katika mpambano wa kukatana shoka wikiendi ijayo katika mchezo wa ligi.Simba iliyocheza na JKT Ruvu ilishinda 2-0 wakati mahasimu wao nao waliweza kushinda 1-0 dhidi ya JKT Oljoro.

NJE   YA NCHI.

UINGEREZA.

Ligi mbalimbali pia ziliendelea katika nchi za nje ambapo nchini Uingereza matokeo ya kushangaza yalikuwa ni kati ya mahasimu Manchester United na Manchester City waliokipiga katika uwanja wa Old Trafford ambapo ilishuhudiwaMan Utd akilala nyumbani kwa mabao 6-1.Lawama za kichapo hicho dhahiri zitamwendea  mlinzi wa Utd Evans aliyemtendea makosa mchezaji wa Man City Mario Balotelli na kuzawadiwa kadi nyekundu mapema katika kipindi cha pili.Matokeo mengine ya ligi ya English Premier League yalikuwa km ifuatavyo;

QPR  1- 0CHELSEA 

ARSENAL 3- 1STOKE CITY 

FULHAM  1- 3 EVERTON  

LIVERPOOL  1- 1NORWICH CITY 


HISPANIA.

MALAGA  0- 4 REAL  MADRID

BARCELONA  0-0 SEVILLA

VALENCIA 1-1 BILBAO.

Sunday, October 16, 2011

Siku ya shukrani kwa familia yetu.




Tunamshukuru Mungu mweza wa yote kwa kuzidi kutulinda na kutujalia kile tunachomwomba katika maisha yetu.Tunasema asante na tunaomba uzidi  kutufanikisha hata katika mahitaji yetu ya kila siku tuyaombayo  kwani wewe ndiwe mpaji wa kila kitu maishani mwetu.  Ni siku nyingine tumekuwa na furaha tele tulipoweza kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki katika kutoa shukrani zetu kwa Mungu kwa yote aliyotutendea  ambapo tulitoa shukrani zetu katika kanisa la kilutheri la mtaa wa Kagondo usharika wa Ibura pia na  hafla ndogo ya kuwakaribisha wapendwa wetu Mama Paulina na Paulina  pamoja na kutupongeza kwa kumaliza masomo ya chuo iliyofannyika katika ukumbi wa Bukoba club.Tunapenda  kuwashukuru kwa uwepo wenu katika yote na Mungu awazidishie mema na moyo huo huo siku zote kwani  undugu siku zote hujengwa na mengi.Pia tunawashukuru ndugu jamaa na marafiki walio mbali nasi kwa maombi yenu kufanikisha siku hii ya leo.Mungu awabariki.

Hapa ni wakati wa kutoa shukrani kanisani.










Ndugu, jamaa  na marafiki tuliosherehekea nao siku yetu.

Saturday, October 15, 2011

Asante Mungu.

Ni vyema kumshukuru Mungu kwa kila jambo na hii haijalishi ni wakati gani bali ni muda wote ule na katika hali yoyote ile hivyo hata uwepo wangu katika blog hii ni kuzidi kumshukuru Mungu kwani nazidi kujifunza na kuyajua mengi kupitia kwa watu mbalimbali ambao wamekuwa na ujuzi na haya mambo nao ni pamoja na wapendwa kaka zangu Mubelwa na Alindwa Bandio pamoja na wengineo wengi ninaopitia kuzisoma blog zao hivyo nazidi kusema asante kwa hilo. Zaidi na zaidi napenda kutoa shukrani zangu kwa familia yangu Baba,Mama,Dadaz na ndugu jamaa na marafiki kwani bila nyie najua nisingeweza kufanya na kukutana na changamoto km hizi. La msingi ni kuzidi kutiana moyo ktk kuimarika hasa katika hiki nilichopendezwa nacho. Mungu awabariki.