Monday, October 29, 2012

UKIMYA ULIOJAA MENGI YA KUSIMULIA MAISHANI.Namshukuru  Mungu kwa kuzidi kuniweka hai na kuzidi kunipigania hata kuiona siku njema na kunijalia hata kuonekana kwa mara nyingine humu baada ya muda mrefu sana.Kiukweli ni ukimya  wa kipindi kirefu sana lakini ni ukimya ambao kiuhalisia una mambo mengi sana kutokana na mambo mbalimbali niliyoweza kupitia kwa kipindi cha miezi kadhaa. HAKIKA   TEMBEA   UONE    na ndivyo ilivyo mpaka sasa kwa upande wangu kwani nimepata fursa ya kujikita katika kazi ambayo kiukweli nimechanja sana mbuga na  kupajua hata nilipokuwa sitegemei kama ningeweza kufika kwa wakati mwafaka.Bado nachanja Mbuga na nitaandika mambo mbalimbali na mabandiko ya kusindikizia kile nikisemacho pale nitapojaliwa kumaliza  mzunguko huu.Much love.

1 comment: