| | |
Dear Mama. | | | |
|
Mama hongera sana kwa kuifikia siku ya leo ambayo unakumbuka siku ya kuzaliwa kwako. Awali ya yote tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kukuzidishia kila lililo jema na hasa afya iliyo njema ya kukufikisha siku ya leo.Tunajivunia sana kuwa na wewe Mama kwani kwa pamoja na Baba mmeweza kutukuza katika malezi yaliyo bora na hata kututimizia kila lililo hitaji katika maisha yetu mpaka leo.Mungu awabariki na kuwazidishia na naamini kabisa kwa pale milipopungukiwa kwa kutuhangaikia wanenu Mungu atapajaza tu. Mama tunakushukuru sana kwa yote na tunazidi kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akuzidishia siku kama hii ya leo nyingi tu huko mbeleni na naamini tutazidi tu kuikumbuka siku hii na kuiheshimu siku zote.Umetufunza mengi na umetukanya mengi ambayo leo hii tunajivunia na kuyatambua.Hakika hakuna kama Mama. Tunakupenda sana Mama na tunakuhitaji sana Mama hivyo tunaomba hata siku hii ya leo iwe ni yetu sote kwa kufurahia ukumbusho wa siku ya kuzaliwa kwako huku tukimshukuru Mungu kwa yote.
 |
Wazazi na watoto wa mwisho ( Mapacha ) |
|
|
|
|
|
|
|
|
 |
Familia. |
Kwa pamoja tunayo furaha kubwa sana kukutakia kila la kheri na uwe na siku njema Mama.
HAPPY BIRTHDAY MAMA.
No comments:
Post a Comment