Kusaidiana siku zote ni kitu cha muhimu hasa pale unapokuwa unauhitaji kwani ni malengo tu ya kujaribu kuyafikia na kuyapunguza mahitaji yako ambayo kwa namna moja ama nyingine yana umuhimu katika kile kinachohitajika kufanyika .Suala langu katika hili leo ni kutaka kuongelea hasa suala la nchi hizi zilizoendelea ambazo ndizo mchango mkubwa sana wa nchi hizi zinazoendelea katika misaada mbalimbali ambayo imekuwa ikipokelewa siku zote na imesaidia katika nyanja mbalimbali japo hii misaada huja na masharti ambayo kwa upande mwingine huonekana kama kutunyonya sana na kuwafaidisha sana hawa watoaji misaada. Katika hili leo nimesikia habari kutoka kwa waziri mkuu wa Uingereza David Cameroon akisema ya kuwa ndoa za jinsia moja zinastahili kuhalalishwa na angalizo hatari ni pale anaposema kuwa kwa zile nchi zinazopokea misaada kutoka katika nchi hiyo zinapaswa kuafikiana na hilo jambo ama sivyo misaada itasitishwa katika nchi husika. Sawa una uwezo na wengi wanakutegemea katika mambo mengi tu ila swali ni je kwakuwa unategemewa na wengi au hata wachache ndio kisa cha kuwafanya wafanye au washabikie hata mambo ambayo kwa wengine ni kukaidi uhalisia wa maisha yao na hata kumkaidi Mungu? Inauma na kusikitisha sana na hapo naoana kama mwisho wa dunia kuelekea kwani hili suala sio la kawaida. Tusimkufuru Mungu hata kama tumejaliwa kuwa navyo jamani.
No comments:
Post a Comment