Kutoka kushoto, Mimi, Michael, Said na Emmanuel katika moja ya hafla tulipokuwa chuoni (May 2011) |
Ni wakati mwingi sana tulikuwa pamoja katika kufanikisha lengo letu la kisomo cha elimu ya juu pale chuoni. Hakika ni suala jema hasa pale tulipomaliza salama ila ilikuwa ni sala zaidi kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja nasi katika kipindi kile chote na hata ushirikiano tulioonyesha baina yetu kama ndugu na naamini tumejenga undugu mzuri tu ambao utadumu daima na Mungu atutangulie katika lyote hasa katika ngwe hii mpya ya maisha.
Kaka Michael Filbert, Emmanuel Kasenga , Said Bakema, Fidelis Choga kiukweli mmekuwa chachu kubwa na nimejifunza mengi kupitia kwenu na hayo naamini nitayafanyia kazi na kuyaendeleza popote pale nitakapokuwa. Pia nawashukuru hata marafiki zangu wapendwa wengi tu japo siwezi kuwataja wote ila ni pamoja na France, Maiko, Said Kingu, Abraham, Willy, Pius, Stanley, Samwel, Gidion, Janeth, Leticia, Ramla, Rachel, Teddy, Debora, Emmy, Naumi, Noela, Tunsume, Julie, na wengineo wengi sana na bila kusahau makundi mbalimbali niliyofanikisha kufanya nayo mijadala mbalimbali juu ya masomo. I do remember you and i love u so so much and keep intouch . Much blessings and all the best.