Tunamshukuru Mungu mweza wa yote kwa kuzidi kutulinda na kutujalia kile tunachomwomba katika maisha yetu.Tunasema asante na tunaomba uzidi kutufanikisha hata katika mahitaji yetu ya kila siku tuyaombayo kwani wewe ndiwe mpaji wa kila kitu maishani mwetu. Ni siku nyingine tumekuwa na furaha tele tulipoweza kujumuika na ndugu, jamaa na marafiki katika kutoa shukrani zetu kwa Mungu kwa yote aliyotutendea ambapo tulitoa shukrani zetu katika kanisa la kilutheri la mtaa wa Kagondo usharika wa Ibura pia na hafla ndogo ya kuwakaribisha wapendwa wetu Mama Paulina na Paulina pamoja na kutupongeza kwa kumaliza masomo ya chuo iliyofannyika katika ukumbi wa Bukoba club.Tunapenda kuwashukuru kwa uwepo wenu katika yote na Mungu awazidishie mema na moyo huo huo siku zote kwani undugu siku zote hujengwa na mengi.Pia tunawashukuru ndugu jamaa na marafiki walio mbali nasi kwa maombi yenu kufanikisha siku hii ya leo.Mungu awabariki.
 |
Hapa ni wakati wa kutoa shukrani kanisani. |
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
 |
Ndugu, jamaa na marafiki tuliosherehekea nao siku yetu. |
Natumai mlikuwa na siku njema.
ReplyDeleteNawapenda nyote na namshukuru Mungu kwa kunifanya mmoja wenu.
BLESS