Monday, October 29, 2012

UKIMYA ULIOJAA MENGI YA KUSIMULIA MAISHANI.



Namshukuru  Mungu kwa kuzidi kuniweka hai na kuzidi kunipigania hata kuiona siku njema na kunijalia hata kuonekana kwa mara nyingine humu baada ya muda mrefu sana.Kiukweli ni ukimya  wa kipindi kirefu sana lakini ni ukimya ambao kiuhalisia una mambo mengi sana kutokana na mambo mbalimbali niliyoweza kupitia kwa kipindi cha miezi kadhaa. HAKIKA   TEMBEA   UONE    na ndivyo ilivyo mpaka sasa kwa upande wangu kwani nimepata fursa ya kujikita katika kazi ambayo kiukweli nimechanja sana mbuga na  kupajua hata nilipokuwa sitegemei kama ningeweza kufika kwa wakati mwafaka.Bado nachanja Mbuga na nitaandika mambo mbalimbali na mabandiko ya kusindikizia kile nikisemacho pale nitapojaliwa kumaliza  mzunguko huu.Much love.

Friday, April 20, 2012

Naikumbuka blog hii na sijaisusa.

Japo bado ni mwanzo tu katika kuangalia ni jinsi gani ninaweza kumudu na kuendeleza kusudi langu la kuwa katika himaya hii ya blog ila naamini palipo na kusudi na nia pia  basi mambo yatatengamaa.Naamini mmekuwa na mwanzo mwema wa mwaka  na mwendelezo mwema pia wa huu mwaka.Tuzidi tu kutakiana kila la kheri na tumtumainie yeye atutiaye  nguvu siku zote.

Wednesday, January 4, 2012

HAPPY BIRTHDAY DAD.

Dad,Mom na  Mapacha.



Tunamshukuru Mungu kwa kuzidi kutulinda na kuzidi kutukirimia afya iliyo njema.Na leo hii tunapokumbuka siku ya kuzaliwa kwako Baba yetu mpendwa tunazidi kukuombea maisha marefu yenye Amani,Upendo na kila aina ya Fanaka.Mungu akubariki nasi tuzidi kujifunza zaidi na zaidi kupitia kwako kama ilivyo kawaida yetu kupitia kwako.Tunakupenda sana Baba.

Thursday, November 17, 2011

HAPPY BIRTHDAY MARTIN. ( 18 NOV )



Katika kuikumbuka siku yako ya kuzaliwa leo tunakutakia kila la kheri na Mungu akujalie maisha marefu yenye AMANI, UPENDO na kila aina ya FANAKA.

HAPPY   BIRTHDAY  MARTIN.

Wednesday, November 16, 2011

HAPPY BIRTHDAY MAMA ( 17 Nov )

   
Dear  Mama.   

Mama  hongera  sana kwa  kuifikia  siku  ya leo ambayo   unakumbuka  siku ya  kuzaliwa kwako.  Awali  ya  yote  tunamshukuru  sana  Mwenyezi  Mungu  kwa  kukuzidishia  kila lililo  jema  na  hasa   afya  iliyo njema   ya  kukufikisha   siku  ya  leo.Tunajivunia  sana  kuwa  na wewe  Mama   kwani  kwa  pamoja  na  Baba  mmeweza  kutukuza  katika  malezi  yaliyo  bora  na  hata  kututimizia  kila  lililo  hitaji  katika  maisha  yetu  mpaka  leo.Mungu  awabariki  na kuwazidishia   na  naamini  kabisa  kwa  pale  milipopungukiwa  kwa kutuhangaikia  wanenu  Mungu atapajaza  tu. Mama  tunakushukuru  sana  kwa yote  na   tunazidi  kukuombea  kwa  Mwenyezi   Mungu  akuzidishia   siku  kama  hii  ya  leo  nyingi  tu  huko  mbeleni  na   naamini  tutazidi  tu kuikumbuka  siku  hii na kuiheshimu  siku zote.Umetufunza   mengi  na  umetukanya  mengi  ambayo leo hii  tunajivunia  na  kuyatambua.Hakika  hakuna  kama  Mama. Tunakupenda  sana  Mama  na   tunakuhitaji  sana  Mama  hivyo  tunaomba  hata siku  hii ya leo  iwe  ni  yetu  sote  kwa  kufurahia  ukumbusho  wa  siku  ya  kuzaliwa  kwako  huku  tukimshukuru  Mungu  kwa   yote. 

Wazazi  na watoto wa mwisho (  Mapacha )








Familia.
Kwa  pamoja tunayo  furaha kubwa sana kukutakia  kila   la kheri   na  uwe  na  siku  njema  Mama.

HAPPY          BIRTHDAY           MAMA.

Tuesday, November 1, 2011

Misaada na laana.


Kusaidiana  siku  zote  ni  kitu  cha  muhimu  hasa  pale  unapokuwa  unauhitaji  kwani  ni malengo tu ya  kujaribu  kuyafikia  na  kuyapunguza  mahitaji  yako  ambayo  kwa  namna  moja  ama  nyingine  yana umuhimu katika  kile kinachohitajika  kufanyika .Suala  langu  katika hili leo ni kutaka kuongelea  hasa suala  la nchi  hizi  zilizoendelea ambazo ndizo mchango  mkubwa  sana wa  nchi  hizi zinazoendelea katika  misaada  mbalimbali  ambayo imekuwa  ikipokelewa  siku zote  na  imesaidia  katika  nyanja  mbalimbali   japo hii  misaada huja  na  masharti   ambayo kwa upande mwingine  huonekana  kama kutunyonya sana na  kuwafaidisha  sana hawa  watoaji  misaada. Katika  hili leo nimesikia  habari   kutoka kwa  waziri  mkuu wa  Uingereza David  Cameroon akisema ya kuwa  ndoa  za jinsia  moja zinastahili kuhalalishwa  na  angalizo hatari ni pale  anaposema  kuwa kwa zile  nchi  zinazopokea misaada  kutoka  katika nchi  hiyo zinapaswa  kuafikiana  na hilo jambo  ama  sivyo  misaada  itasitishwa  katika nchi husika. Sawa  una  uwezo  na wengi wanakutegemea  katika  mambo mengi  tu ila swali ni  je  kwakuwa  unategemewa  na  wengi au hata  wachache ndio  kisa  cha kuwafanya wafanye au washabikie  hata mambo ambayo  kwa wengine ni  kukaidi uhalisia wa maisha yao na hata kumkaidi  Mungu?  Inauma na kusikitisha  sana na  hapo  naoana kama mwisho  wa dunia kuelekea  kwani hili suala sio  la  kawaida.  Tusimkufuru  Mungu  hata kama tumejaliwa kuwa navyo jamani.